Umoja wa Mataifa watoa wito wa kupelekwa misaada ya kibinadamu Pakistan
Umoja
wa Mataifa umetoa wito kwa nchi na mashirika mbalimbali kote
ulimwenguni kujitokeza kwa wingi na kutuma misaada nchini Pakistan,
ambako mvua kubwa inayoendelea kunyesha, imesababisha vifo vya zaidi ya
watu 1000. Duru kutoka nchini humo zimeripoti kuwa, idadi ya walioaga
dunia kutokana na mafuriko hayo imepanda na kufikia 1,300 huku maelfu
ya wengine wakiwachwa bila makao. Shirika la Afya Duniani WHO
linaendelea kutoa matibabu ya dharura kwa waathiriwa mjini Peshawar.
Mapema leo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa itatuma misaada ya
dharura kwa waathiriwa wa janga hilo. Idara ya Hali ya Anga nchini humo
imesema, mvua hiyo inatarajiwa kuendelea kunyesha zaidi katika maeneo
mbalimbali nchini Pakistan. Janga hilo la kimaumbile linaaminika kuwa
kubwa zaidi kuwahi kuikumba Pakistan tangu mwaka wa 1929.
0 comments:
Post a Comment