Rais Hosni Mubarak wa Misri amesema nchi yake inajiandaa kujenga kituo chake cha kwanza cha kuzalisha nishati ya nyuklia. Kupitia Msemaji wake Suleiman Awadh, Rais Mubarak amesema kuwa kituo hicho cha kuzalisha nishati hiyo muhimu kitajengwa mjini El-Dabaa, katika pwani ya magharibi ya badari ya Alexandria. Serikali ya Misri inatarajia kituo hicho kuanza shughuli zake kufikia mwaka wa 2019. Katika safari yake nchini Misri mwezi Juni, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA Yukiya Amano alisema kuwa, wakala huo uko tayari kuisaidia nchi hiyo kunufaika na nishati ya nyuklia. Misri ilitia saini Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia NPT mwaka wa 1981.
*****************************
I |
Iran yasema kuwa Marekani ndio mfadhili
mkubwa wa uhaini duniani
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa utawala wa kibeberu wa Marekani ndio mfadhili mkubwa wa viongozi wahaini ulimwenguni na wachochezi wa ghasia zilizogubika nchi kadhaa baada ya kufanyika chaguzi katika nchi hizo. Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran ya Kiislamu Heidar Moslehi ameviambia vyombo vya habari kuwa, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na wizara yake, Marekani ilitumia takriban dola bilioni moja kufadhili machafuko yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu hapa nchini mwaka jana. Amesema kuwa, licha ya ufadhili na uchochezi uliofanywa na Marekani baada ya uchaguzi huo, maafisa usalama wa Iran waliweza kukabiliana na njama kubwa zilizokuwa zimepangwa na nchi hiyo. Moslehi ameongeza kuwa, Marekani ndiyo iliyowapa nguvu vibaraka walioongoza machafuko hayo nchini.
0 comments:
Post a Comment