Jonathan azidi kuungwa mkono Nigeria
Chama tawala cha Nigeria kimekubali kuwa Rais Goodluck Jonathan ana haki ya kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao, hatua hiyo ikiwa kinyume na sheria ya chama.
Chama cha People Democrat PDP kina kanuni isiyoandikwa ya kubadilishana madaraka baina ya upande wa kusini na kaskazini mwa nchi hiyo.
Bw Jonathan, ambaye ni wa kusini, alishika wadhifa wa urais, mrithi wake alipofariki dunia takriban nusu ya muda wa upande wa kaskazini wa mihula miwili ya urais kukamilika.
PDP imeongoza Nigeria tangu irejee kwenye uongozi wa kidemokrasia mwaka 1999.
Nigeria, nchi barani Afrika inayoongoza kwa uzalishaji wa mafuta na taifa maarufu, ina historia ya mapinduzi, na ghasia za kidini pamoja na za kikabila.
Bw Jonathan aliapishwa kuwa Rais kufuatia kifo cha Umaru Yar'Adua baada ya kuugua kwa muda mrefu mwezi Mei 2010.
Mwenyekiti wa PDP Okwesilieze Nwodo alisema, " Chama kinaamini Dr Goodluck Jonathan ana haki ya
kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2010."
Lakini aliongeza kuwa hatua hiyo haitomzuia mwengine yeyote kutoka chama cha PDP kuwania nafasi hiyo.
Siku mia moja
Bw Jonathan bado hajasema iwapo atawania nafasi hiyo au la.
Waandishi wanasema kuibuka kwake kutoka kuwa naibu gavana asiyejulikana, ambaye hakuwa na misingi yeyote ya kisiasa, mpaka kuwa Rais imekuwa nyepesi.
Baada ya kupita miezi kadhaa huku siasa za nchi hiyo zikiwa na utata kutokana na kuugua kwa Bw Yar'Adua, wengi walifurahi kuona Bw Jonathan akichukua nafasi hiyo.
Hata hivyo, mwandishi wa BBC Ahmed Idris aliyopo mji mkuu wa Abuja, amesema siku 100 alizokuwa madarakani mpaka sasa umaarufu wake umeanza kupungua.
Amesema watu wanahisi mjadala wa iwapo ataweza kuwania uchaguzi mwaka 2011, unaotarajiwa kufanyika mwezi Januari, umepewa umuhimu zaidi kuliko kushughulikia masuala muhimu kama vile kupambana na rushwa, tatizo la umeme na urekebishaji wa uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment