Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya uungaji mkono wa serikali na wananchi wa Iran kwa taifa la Lebanon katika kukabiliana na vitisho vinavyotolewa mara kwa mara na adui Mzayuni. Akizungumza na Ali ash Shami Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Lebanon mjini Tehran, Rais Ahmadinejad amewasifu wananchi wa Lebanon katika kusimama kwao kidete katika kukabiliana na vitisho vya utawala wa Israel na kuongeza kuwa, Lebanon ikiwa ni nchi iliyo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya siasa za kutaka kujitanua za Wazayuni, inapata uungaji mkono kamili wa nchi za Kiislamu za eneo la Mashariki ya Kati, ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Rais wa Iran ameongeza kuwa, umoja na mshikamano ulioko leo hii kati ya shakhsia na makundi mbalimbali ya Lebanon bila shaka utabadilisha mlingano wote kwa maslahi ya muqawamah na wananchi wa eneo hili. Kwenye mazungumzo hayo, naye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Lebanon ameishukuru misimamo ya Iran katika kukabiliana na satua za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo.
Monday, August 9, 2010
Ahmadinejad asisitiza uungaji mkono wa Iran kwa taifa la Lebanon
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, August 09, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment