Afrika Kusini imesema kuwa inataka kuorodheshwa kwa njia isiyo rasmi katika kundi la BRIC linalozijumuisha nchi za Brazil, Russia, India na China. Lengo kuu la kundi la BRIC ambalo linaongoza mataifa yanayokuwa kiuchumi, ni kuhakikisha mataifa yanayokuwa kiuchumi yanashirikishwa katika masuala ya uchumi wa ulimwengu na kupata sauti kwenye mashirika ya kimataifa kama lile la Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF. Zuma ambaye yuko ziarani nchini Uchina tayari ameshazuru nchi za Brazil, Russia na India katika jitihada za kutafuta uanachama katika kundi la BRIC. Rais huyo amesema kuwa, juhudi zake za kutafuta uanachama huo zinatokana na ukweli kwamba hakuna hata nchi moja ya Afrika ambayo ni mwanachama wa kundi hilo. Baadhi ya wadadisi wa masuala ya kiuchumi wanaona kuwa, uchumi wa wanachama wa BRIC unakuwa kwa kasi na unatazamiwa kuupiku ule wa mataifa 8 yaliyostawi kiuchumi ya G8.
Thursday, August 26, 2010
Afrika Kusini yataka kuungana na kundi la Mataifa ya BRIC
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, August 26, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment