Waziri Mkuu wa Somalia abadilisha mawaziri, walinda amani wauawa
Waziri Mkuu wa
Somali amewateua mawaziri wawili kutoka Harakati ya Ahlu Sunna Waljamaa
hata hivyo kundi hilo limewapinga walioteuliwa.
Ahmed Abdi Salan ameteuliwa kuwa waziri wa usalama naye Yusuf Dhulow ameteuliwa kuwa waziri wa mipango na ushirikiano wa kimataifa. Wote wanasemekana kuwa wanachama wa Ahlu Sunna Waljamaa lakini kundi hilo limepinga uteuzi huo. Msemaji wa Ahlu Sunna Waljamaa Sheikh Abdullahi Sheikh Abu Yusuf amesema mawaziri hao hawawakilishi kundi hilo linalowajumuisha Waislamu wenye itikadi za Kisufi. Katika mabadiliko hayo ya braza la mawaziri Waziri Mkuu Omar Abdirashid Sharmarke pia amemteua Yusuf Ibrahim Hassan kuwa Waziri wa Mambo ya Nje huku Abubakar Abdi Osman akipewa wadhifa wa Waziri wa Ulinzi. Wakati huo huo askari wawili raia wa Uganda katika Kikosi cha Kulinda Amani wa Umoja wa Afrika AMISOM wameuawa mjini Mogadishu. Msemaji wa AMISOM Barigye Ba Hoku amesema askari hao waliuawa alhamisi walipokuwa wakilinda doria.

0 comments:
Post a Comment