Timu ya Taifa ya Uhispania imefuzu kuingia nusu fainali ya Kombe la
Dunia mwaka 2010 baada ya kuifunga Paraguay bao(1) moja kwa bila(0) katika
mechi iliyochezewa uwanja wa Ellis Park mjini Johannesburg.
Bao hilo lilipachikwa wavuni na David Villa kunako dakika ya 82 katika mechi hiyo iliyokuwa ngumu kwa Paraguay ambao walikosa penati.
Uhispania sasa
itachuana na Ujerumani ambayo nayo iliingia nusu fainali ya mashindano
hayo baada ya kuigaragaza bila huruma timu ya soka ya Argentina mabao
4-0. Mechi kati ya Ujerumani na Uhispania itachezwa Jumatano baada ya
ile ya Uruguay na Uholanzi itakayochezwa Jumanne. Kuingia timu tatu za
nchi zilizostawi za Ulaya katika nusu fainali ya Kombe la Dunia
kumewasikitisha mashabiki wa soka waliokuwa wakitaraji maeneo mengine ya
dunia kupata fursa ya kusonga mbele katika michuano hiyo.
katika mechi hiyo mchezaji ANDRES INIESTA wa timu ya Uhispania alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Bao hilo lilipachikwa wavuni na David Villa kunako dakika ya 82 katika mechi hiyo iliyokuwa ngumu kwa Paraguay ambao walikosa penati.
David
VILLA
katika mechi hiyo mchezaji ANDRES INIESTA wa timu ya Uhispania alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
ESP-Andres
INIESTA
0 comments:
Post a Comment