SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, July 3, 2010

Ujerumani yaitimua nje Argentina yaidhalilishwa kwa kuitandika 4 - 0


Arne Friedrich of Germany (2L) celebrates scoring the third goal 
with teammates Miroslav Klose (L), Thomas Mueller (2R) and Per 
Mertesacker

Timu ya taifa ya soka ya Ujerumani imetinga nusu fainali ya mashindano ya soka ya kombe la dunia kwa kishindo, baada ya kuigaragaza bila huruma timu ya soka ya Argentina mabao 4-0. 
Ushindi huo mkubwa wa Ujerumani ni wa tatu baada ya kuifunga Australia mabao 4-0 na Uingereza mabao 4-1 na kuitoa timu hiyo katika mashindano hayo. Ujerumani ikicheza kandanda safi iliwapeleka mchakamchaka vijana wa Argentina walioko chini ya ukufunzi wa kocha Diego Maradona. 
Kikosi cha Ujerumani kilichoitumua Argentina 4:0
Kikosi cha Ujerumani kilichoitumua Argentina 4:0
Mambo yalianza kuwaendea kombo Argentina mapema baada ya Muller kupachika bao la kwanza katika dakika ya tatu tu ya mchezo. 
Kwa ushindi huo Ujerumani sasa inasubiri mshindi wa mechi ya baadaye leo baina ya Uhispania na Paraguay katika kindumbwendumbwe cha nusu fainali ya kombe la dunia, mashindano yanayoendelea huko nchini Afrika Kusini.
Miroslav KLOSE 
Miroslav KLOSE
Argentina iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe la dunia mwaka huu imefungasha virago na kuyaaga mashindano hayo kwa uchungu na hivyo kuungana na timu zingine kubwa zilizotolewa mapema katika mashindano hayo kama Ufaransa, mabingwa watetezi Italia, Uingereza na Brazil.
katika mechi hiyo mchezaji BASTIAN SCHWEINSTEIGER wa timu ya Ujerumani alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
GER-Bastian SCHWEINSTEIGER

0 comments:

Post a Comment