Rafael Nadal kutoka Uhispania
ndiye bingwa wa mwaka huu wa 2010, mashindano ya tennis ya Wimbledon ya
Uingereza.
Rafael
Nadal ndiye bingwa mpya wa Wimbledon
Nadal, Jumapili, alimshinda mpinzani wake katika
fainali ya wanaume, Tomas Berdych kutoka Jamhuri ya Czech, kwa 6-3 7-5
na 6-4.
Mchezaji huyo alisema ushindi huo ulikuwa ni
zaidi ya ndoto aliyokuwa nayo kuhusu fainali hiyo, hasa kwa kuwa
alitamani sana kuwa katika mashindano ya Wimbledon mwaka jana, lakini
hakuweza kushiriki.
Alisisitiza kushiriki katika mashindano ya mwaka
huu, na kuondoka na tuzo, bila shaka ni zaidi ya ndoto.
Hii ni mara ya pili Nadal amefanikiwa kutwaa
ubingwa wa mashindano ya Wimbledon, yanayofanyika kusini-magharibi mwa
mji wa London.
Nadal, ambaye kwa sasa hivi ndiye mchezaji bora
zaidi wa kiume ulimwenguni, alimshinda mpinzani wake Berdych kwa ushindi
wa moja kwa moja katika seti zote.
Mwaka uliopita wa 2009, Nadal hakuweza kuutetea
ubingwa wake kutokana na jeraha.
Kwa jumla, Nadal kufikia sasa amewahi kuwa
bingwa katika mashindano manane makubwa, yaani Grand Slam.
Katika mashindano ya kina dada, Serena Williams
kutoka Marekani aliweza kuwa bingwa wa Wimbledon aliposhinda katika
fainali iliyochezwa siku ya Jumamosi.
*************************
*************************
| Kocha Dunga avuliwa ukufunzi wa Brazil |




0 comments:
Post a Comment