Waliokufa shambulio la bomu Uganda ni 74
Idadi ya watu waliokufa katika
mashambulio mawili ya mabomu yaliyotikisa wakati mashabiki wakiangalia
mechi ya fainali ya Kombe la Dunia mjini Kampala huko Uganda,
imeongezeka kufikia 74, maafisa wanasema.
Watu wengine 70 walijeruhiwa katika mashambulio
hayo yaliyolengwa klabu ya mchezo wa raga ya Kampala na mgahawa mmoja wa
vyakula vyenye asili ya Ethiopia.
Ingawa wanamgambo wa Al Shabab wamekiri
kuhusika, polisi wanachunguza endapo walifanya mashambulio ya kujitolea
muhanga.
Kulinda amani
Wanajeshi wa kulinda amani wa Uganda wanatumikia
nchini Somalia, na al-Shabab wametishia kushambulia Kampala katika siku
zilizopita.
Takriban askari 5,000 wa kulinda amani wa Umoja
wa Afrika kutoka Uganda na Burundi wapo Mogadishu kusaidia serikali ya
mpito ambayo si imara.
Jeshi la AU nchini Somalia (Amisom) limekuwa
likikabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo
wanaodhibiti sehemu kubwa ya kusini na katikati ya Somalia.
Mashambulio yote mawili yalisababisha vifo na
majeraha, ingawa watu wengi zaidi walikufa kwenye klabu ya mchezo wa
raga, ambako mashabiki walikuwa wakifuatilia mechi hiyo kupitia skirini
kubwa.
bbc swahili.
0 comments:
Post a Comment