Msemaji wa
kundi lenye misimamo mikali la Al Shabab la Somalia amekiri kuwa kundi
hilo limehusika na mashambulizi mawili ya mabomu yaliyolenga watu
waliokuwa wakitazama fainali ya Kombe la Dunia jana usiku mjini Kapala,
Uganda. Ali Muhammad Rage amesema kundi la Al Shabab limehusika katika
mashambulizi hayo na kwamba iwapom askari wa Uganda wataendelea kuua
Wasomali basi kundi hilo litaendelea mashambulizi yake. Amedai kwamba
mashambulizi hayo yamefanywa kulipiza kisasi cha mauaji ya Wasomalia
wanaouawa na askari wa Uganda. Wakati huo huo kamanda wa ngazi za juu wa
kundi la Al-shabab amesema kuwa amefurahishwa mno na milipuko miwili ya
mabomu iliyotokea usiku wa jana mjini Kampala Uganda na kusababisha
vifo vya watu 74. Sheik Yusuf Sheik Issa amesema kuwa Uganda ni adui wa
kundi hilo na chochote kinachoiliza nchi hiyo basi ni furaha kwa
Al-shabab. Makumi ya watu pia walijeruhiwa kwenye milipuko ya jana
iliyotokea wakati watu walipokuwa wakitazama mechi ya fainali ya Kombe
la Dunia kati ya Uhispania na Uholanzi. Rais Yoweri Museveni wa Uganda
ametoa mkono wa pole kwa wahanga wa mashambulio hayo na kuahidi kuwa
serikali itafanya juu chini kuwatia nguvuni waliohusika.
Iwapo
itabainika kuwa Al Shabab imehusika basi itakuwa mara ya kwanza kwa
kundi hilo kufanya mashambulizi nje ya mipaka ya Somalia. |
0 comments:
Post a Comment