SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, July 22, 2010

WAKAZI WA KUNDUCHI MTONGANI WACHARUKA


Wakazi wa Kunduchi wakiwa wamelala barabarani.
WAKAZI wa Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam, leo walizua kizazaa baada ya kuifunga barabara kuu inayotoka Mbuyuni kuelekea eneo hilo kufuatia gari aina ya Toyota Hiace linalofanya shughuli za daladala kati ya Kunduchi na Mwenge kuwagonga na kuwaua watoto wawili wa familia moja. Vurugu hizo zilisababisha askari wa kutuliza ghasia FFU, kutumia mabomu ya kutoa machozi ingawa baadaye walikatazwa kutumia mabomu hayo na askari wa JWTZ wa kambi iliyopo jirani na eneo hilo kutokana na muingiliano wa mionzi kati ya mabomu hayo na vifaa vyao.
Dereva wa pikipiki (mwenye fulana ya pundamilia) akipewa kichapo na akina mama baada ya kutaka kupita kinguvu eneo lililofungwa.
Hata magari ya dharura kama Tanesco nayo yalipigwa stop kutumia barabara hiyo. 
Wakazi wenye hasira wakimshusha kinguvu abiria mmoja aliyepakizwa pikipiki na kutaka kukatiza eneo hilo. 
Akina mama wakimueleza kilio chao afisa mmoja wa polisi aliyekuwa akiwataka kuacha vurugu. 
Barabara ikiwaka moto baada ya wananchi kuchoma matairi ya gari katikati ya barabara. 
Kina mama wakiwa barabarani na vidumu na chupa za maji ya kunawa uso endapo watapigwa mabomu ya mchozi. 
Askari Polisi akijaribu kuzima moto, moja ya tairi lililowashwa barabarani. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elius Kalinga akiwatuliza wananchi wenye munkari na kuwaambia kuwa serikali inashughulikia suala la kuweka matuta barabara hiyo. 
Naibu Kamanda Mkuu wa Polisi, Kanda maalum ya Dar es Salaam, Charles Kenyela naye alifika eneo la tukio na kuwatuliza wanacnhi wenye jazba. 
Askari wakiwa tayari kwa lolote. 
PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL 

0 comments:

Post a Comment