SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, July 21, 2010

MR. NICE UKO WAPI.....!!!!!!!
NGOMA YA MR. NICE BWANA SHAMBA

Ukizungumzia jina la MR.NICE kwa jina la la kuandikishwa ni "NICE LUCAS NKENDA" si jina geni miongoni mwa wadau wa muziki wa kizazi kipya,kama anavyofahamikaka zaidi kwa mashabiki na wapenzi wa bongo Flava. Aliiteka vilivyo medani hii ya muziki wa kizazi kipya kwa staili yake ya kipekee iitwayo "TAKEU" Alijijingea jina na heshima kubwa nchini Tanzania na kupendwa na watu wa lika zote kuanzia Watoto,Vijana na Wazee na kuteka mashabiki na wapenzi wengi katika muziki wake kutokana na umahiri wake wa kuimba na kukamua vilivyo pindi anapopanda jukwaani.Si hivyo tu bali aliweza kuliteka soko la muziki la Afrika Mashariki na Kati na sehemu nyingine za Afrika. Pia aliweza kutesa na kushika na nje ya Bara la Afrika na kupata shoo na mialiko mingi katika nchi mbalimbali za ulaya na Amerika kifupi jamaa yuko "FULL" sana kuimba na kucheza vyote kwa wakati mmoja akipanda jukwaani huvifanya na kuwashika vilivyo mashabiki na wapenzi wa muziki wake.
nicebc.jpg (403×336)
 SWALA LA MSINGI LINAKUJA KWAKO KAKA UKO, WAPI NA UNAFANYA NINI KATIKA KIPINDI HIKI CHOTE  
SABABU MASHABIKI NA WAPENDA MUZIKI WAKO WAMEKUWA MARA KWA MARA WAKIULIZIA  JUU YAKO, UKO WAPI,NA UNAFANYA NINI HUKO ULIPO
NAKUTAKIA KILA LA HERI HUKO ULIPO MOLA AKUJAALIE  NA IMANI IPO DAY  MOJA MAJIBU YA HAYA MASWALI UTAYAJIBU KUPITIA HAPA 24SEVEN 365.
IMEANDIKWA NA ALLY S. MGIDOS

0 comments:

Post a Comment