Kuanzishwa Mahakama ya Kadhi nchini Tanzania bado kitendawili:
Suala la kuanzishwa Mahakama ya Kadhi nchini Tanzania, linaonekana kuwa bado ni kitendawili ambacho hakijateguliwa.
Jana Jopo la Masheikh na wanasheria
Waislamu, lilitangaza hoja tatu muhimu ambazo ni sehemu ya hoja
zitakazorejeshwa serikalini, kufanyiwa kazi zaidi kabla ya kuanzishwa
kwa Mahakama ya Kadhi nchini Tanzabnia.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Issa Shaabani Simba ambaye ni Mwenyekiti wa jopo hilo lenye wajumbe 25,
amesema kuwa, kabla ya kubainisha hoja hizo, walipokea na kujadili
mapendekezo kuhusu namna ya uanzishwaji wa mahakama hiyo.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika Ofisi za Baraza la Waislamu Tanzania
(Bakwata) jana, Mufti Simba amesema, mapendekezo hayo yalipelekwa kwao
kutoka katika kikao cha Sekretarieti ya Serikali na Waislamu. Kati ya
mambo hayo ambayo masheikh hao wanataka kujadili upya na Serikali,
Sheikh Simba alitaja hoja inayohusiana na gharama za uendeshaji wa
mahakama hiyo na namna Uamuzi wa mahakama hiyo utakavyokuwa na nguvu ya
kisheria.
Hoja nyingine ya tatu iliyotajwa na Sheikh Simba inahusu jinsi
Mahakama ya Kadhi, itakavyoingizwa katika mfumo wa mahakama nchini
Tanzania
0 comments:
Post a Comment