Raia wa jamuhuri ya kidemokrasia
ya Congo wanaanza siku mbili ya maombolezi ya kitaifa, kufuatia vifo
vya watu mia mbili thelathini kwenye mlipuko wa lori ya mafuta mashariki
mwa nchi hiyo.
Kuna hofu kuwa idadi hiyo ya maafa ikaongezeka.
Madaktari mkoani Kivu wanaendelea kuwahudumia
mamia ya majeruhi wa ajali hiyo huku hospitali nyingi zikikumbwa na
wakati mgumu kutoa huduma bora kutokana na uhaba wa vifaa vya matibabu.
Hapo Jumamosi waathiriwa 200 walizikwa kwenye
kaburi la pamoja. Bendera za nchi hiyo zinapeperushwa nusu mlingoti.
Katika hotuba kwa taifa hilo, rais wa nchi hiyo
Joseph Kabila amesema wamepokonywa ndugu na dada kwa njia ya kikatili.
Lori hilo la mafuta lilianguka katika kijiji cha
Sange siku ya Ijumaa wiki iliyopita.
Wakati watu walipokuwa wakijaribu kuteka mafuta
yaliyokuwa yakivuja, lori hilo lililipuka na kusababisha moto mkubwa
ulioteketeza nyumba kadhaa na kusababisha vifo hivyo.
0 comments:
Post a Comment