Rais Luiz Lula
da Silva wa Brazil ameshiriki kwenye kikao cha Jumuiya ya Ustawi ya
Magharibi mwa Afrika ECOWAS nchini Cape Verde na kusisitiza juu ya
kuimarishwa uhusiano wa pande zote kati ya nchi hiyo na bara la Afrika.
Akizungumza mbele ya wakuu wa nchi kumi wanachama wa ECOWAS, Rais da
Silva amesisitiza juu ya kuhifadhiwa umoja na kupigwa hatua za
kimaendeleo. Amesema kuwa, licha ya kuwa hivi sasa Brazil haina wenzo
mkubwa wa kisiasa, lakini ina suhula nzuri za kiuchumi na utaalamu wa
kiufundi, ambazo zinaweza kutumiwa vyema na nchi za Kiafrika. Hadi sasa
Rais Lula da Silva ameshazitembelea nchi 25 za Kiafrika tokea aingie
madarakani, na baada ya kuondoka Cape Verde, Rais Lula da Silva
ameelekea Equatorial Guinea, na leo anatarajiwa kuwasili nchini Kenya,
na baada ya hapo ataelekea Tanzania, Zambia na hatimaye nchini Afrika
Kusini ambako atashiriki kwenye sherehe za kumalizika kwa michuano ya
kombe la dunia nchini humo siku ya Jumapili ijayo. Rais wa Brazil
atashiriki kwenye sherehe hizo, huku timu ya nchi yake tayari
imeshayaaga mashindano hayo, baada ya kutandikwa na Uholanzi mabao 2 kwa
1 kwenye mechi ya robo fainali. |
0 comments:
Post a Comment