Bronislaw Komorowski na mkewe Anna.
Bronislaw Komorowski, ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais
uliofanywa siku ya Jumapili nchini Poland.
Kwa mujibu wa televisheni ya taifa TVP, Komorowski
amejikingia asilimia 53 ya kura zilizopigwa wakati mpinzani wake,
Jaroslaw Kaczynski amepata asilimia 47.
Kaczynski ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani
kinachofuata sera za mrengo wa kulia, "Law and Justice" na ni ndugu
pacha wa rais Lech Kaczynski alieuawa katika ajali ya ndege mwezi wa
Aprili.Uchaguzi wa rais umeitishwa kufuatia kifo hicho.
Matokeo ya uchaguzi huo humaanisha kuwa Komorowski wa
chama cha kiliberali cha "Civic Platform" na mshirika wake wa karibu,
Waziri Mkuu Donald Tusk wataweza kuidhinisha marekebisho ya kifedha
kabla ya uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanywa mwakani.
Waziri
Mkuu wa Poland,Donald Tusk.
Kwa mujibu wa Katiba ya Poland, wajibu wa rais sio
kuliwakilisha taifa tu bali ana mamlaka yake hasa katika sera za nje na
usalama. Jaroslaw Kaczynski amekubali kuwa ameshindwa na amempongeza
mpinzani wake Komorowski.
Mwandishi:P.Martin
0 comments:
Post a Comment