SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, July 17, 2010

SAKATA LA WIMBO “NITAFANYA”-KIDUM ATOA MAELEZO YAKE
Kufuatia  kutoelewana kulikoibuka kuhusiana na wimbo Nitafanya wa wanamuziki Kidum na Lady Jaydee na Producers wa wimbo huo Hermy B(original version) na RKay Kamanzi(second version),tumepokea maelezo kutoka kwa Kidum.Bila kuyahariri tunayaweka hapa chini;
Mimi ni Kidum .Nataka kutoa maelezo kikamilifu kuhusiyana na iyi muzozo wa uyu wimbo wangu na Lady Jaydee .Hakuna shida yeyote yipo kati yangu na Hermy B ambayo ni producer wa round ya kwanza ya recording ya uyu wimbo .
Kama vile munajuwa mimi naishi nairobi na hapa ndipo nafanya shuhuli za muziki wangu kwa muda mrefu .Sasa kama kwa mfano nime rekodi Dar es salaam alafu nisikiye kuna hitirafu kidogo kwa wimbo ni ngumu niwe nachukuwa ndege kila mara nikikuja Dar es salaam ingawa napapenda sana wakati hapa nairobi pia kuna studios .
Kwa mfano version ya kwanza Key ile tuliimbiya mimi na jaydee ni yenye ambao ilikuwa chini sana kuweza kuwa rahisi kwa mwana dada lakini tulipo rudiya sasa mwana Dada sauti yake ikatoka kama ya malaika .Hapakuwa ubaya wakurudiya ku rekodi tena uyu wimbo sababu mimi mwenyewe niko msanii na kuna kile kitu mimi natafuta kwa hali ya ubora zaidi kama sikipati bila shaka ata ku rekodi mara ya tatu siwezi kusita kufanya . Wimbo ni wangu mimi na lady jaydee sisi wenyewe tukielewana na tuamue kurudia sioni kama kuna ubaya .Hata Hermy B mwenyewe na amini munamusemeya uwongo ya kwamba anamatatizo kuhusiyana uyu wimbo sababu mimi mwenyewe naelewa vema kwenye radio stations nyingi wanacheza version yake ya Audio . bado ni uyo wimbo tu iwe video ama audio .Na pia bado ni Kidum na Lady Jaydee iwe ni video ama ni Audio.  bongocelebrity.com

0 comments:

Post a Comment