Rais wa Congo akutana na familia za wahanga wa mlipuko wa lori la mafuta
Rais Kabila alitangaza siku mbili za maombolezo ya nchi nzima baada ya kutokea ajali hiyo. Viwiliwili visivyopungua sitini vingi kati ya hivyo vikiwa vya watoto, vilizikwa kwenye makaburi matatu ya halaiki siku ya Jumamosi iliyopita. Viongozi wa Congo bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
**************************
Clinton aitahadharisha Washington juu ya kuiwekea mashinikizo Iran
Bill Clinton Rais Mstaafu wa Marekani amesema kuwa, kuendelezwa mashinikizo na vikwazo zaidi dhidi ya Iran kuhusiana na miradi yake ya nyuklia yenye malengo ya amani, kutakuwa na matokeo mabaya katika siku zijazo. Clinton amesisitiza kuwa, Iran ni moja kati ya nchi zilizotia saini mkataba wa kuzuia kuzalisha na usambazaji silaha za nyuklia NPT, na katika miaka kadhaa iliyopita licha ya kuheshimu sheria za kujipatia teknolojia hiyo muhimu, imekuwa ikisisitiza kwamba miradi yake ya nyuklia inafanyika kwa malengo ya amani. Rais Mstaafu wa Marekani ameonya hatua yoyote ya kutolewa mashinikizo zaidi dhidi ya Iran.




0 comments:
Post a Comment