Mkuu
wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa matumizi ya
teknolojia ya Long Term Evolution - LTE leo jijini Dar es salaam. Kulia
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza na kushoto ni
Mtaalamu kutoka Nokia Siemen Surender Surana. Vodacom imezindua matumizi
ya LTE kwa majaribio katika eneo la Msasani jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa Idara ya Uhandisi wa kampuni ya Vodacom George Magonyozi akielezea
jambo wakati wa uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya Long Term
Evolution - LTE kwa mawasiliano ya mtandao wa Vodacom leo jijini Dar es
salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene
Meza (katikati) na Ofisa Mkuu wa Mtandao Alec Mulonga wakimsikiliza kwa
umakini. Vodacom imezindua matumizi ya LTE kwa majaribio katika eneo la
Msasani jijini Dar es salaam.
Mwaandishi wa habari wa Clouds TV Suleiman Masoud (kulia) akishuhudia namna ya huduma ya intaneti iliyounganishwa na teknolojia ya Long Term Evolution - LTE inavyofanyakazi kwa kasi, Vodacom imezindua matumizi ya LTE kwa majaribio katika eneo la Msasani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waandishi wa habari wakifuatilia majaribio ya uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya Long Term Evolution - LTE jijini Dar es salaam.
----
Taarifa kwa vyombo vya habari
VODACOM YAANZA MAJARIBIO MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA LTE
* Wateja maeneo ya Msasani kuanza kunufaika
Dar es Salaam, January 30, 2013 ... Wateja wa Vodacom sasa wanauwezo wa kutumia teknolojia ya Long Term Evolution - LTE ambayo ni ya kisasa zaidi ulimwenguni katika utoaji wa huduma za Mawasiliano na hivyo kupunguza gharama katika kuwasiliana kufuatia kampuni hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Nokia Siemens kuwawezesha wateja wake kufanya hivyo katika mradi wa majaribio unaohusisha eneo la Msasani jijini Dar es salaam.
Majaribio hayo yanafanywa kwa ushirikiano na kampuni ya Nokia Siemens yatahusisha eneo lote la Msasani jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwawezesha wateja wa kampuni hiyo kuona ubora wa teknolojia hiyo katika kupokea huduma za simu za mkononi ikiwemo kupiga simu, kutumia huduma za Intaneti n.k
"Ni hatua nyingine muhimu kutoka Vodacom tunapowawezesha wateja wetu kupata kile ambacho ni wazi kitawapunguzia gharama katika matumizi ya huduma zetu sokoni bila ya kuwepo na mabadiliko ya gharama."Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wakati akitangaza rasmi kuanza kwa majaribio hayo leo jijini Dar es salaam
LTE inayofahamika pia kwa jina la 4G ndio teknolojia ya kisasa zaidi ulimwenguni ambayo imedhihirisha uwezo wa hali ya juu katika mawasiliano ikiwemo huduma za intanteti katika kudadavua mitandao kupata filamu, machapisho, michezo ya kwenye kompyuta n.k
"Kwetu sisi kuwawezesha wateja wetu kuweza kuijaribu teknolojia bora na ya kisasa zaidi ni kielelezo cha namna ambavyo Vodacom inavyoishi kimatendo kwa dira yake katika kuongoza mageuzi katika sekta ya huduma za simu za mkononi nchini."Alisema Meza na kuongeza kuwa "Tunaona fahari kubwa namna kampuni yetu inavyokwenda sanjari na wimbi la mabadiliko ya teknolojia lililopo katika muktadha wa utandawazi, na namna inavyozitumia kwa ufasaha faida za kiteknolojia siku hadi siku katika kukidhi matakwa ya wateja wake.
Meza amesema Vodacom imeanza na Msasani kutokana na eneo hilo kuwa na uwiano mzuri wa shughuli za kibiashara na makazi ambazo zote zinahitaji huduma za Intaneti zenye kasi za kiwango cha LTE ingawa mipango ni kuisambaza teknolojia hiyo katika maeno mengine nchini
"Tunatambua kuwa njia za masafa ya hewa ya mawasiliano kwa mfumo wa LTE kwa sasa zimejaa hapa nchini hata hivyo bado Tanzania haijafikiwa kwa ukamilifu na huduma za Intaneti zenye kasi, hivyo basi ni matumaini yetu kwamba serikali itatupatia muongozo ili nasi kupitia mtandao mpana wa Vodacom tuwwawezeshe watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za Teknohama zenye ubora unaoendana na mahiraji ya sasa."
Kwa upande wake, Mkuu wa huduma za Vodacom katika kampuni ya Nokia Siemens Pete Beadle, alisema kiwango cha juu cha teknolojia za mawasiliano ndani ya kampuni hiyo duniani kote imekuwa ni chaguo la majaribio kwa kampuni zinazotoa huduma zinazozingatia teknolojia za kisasa, kutokana na dhana yake ya mwingiliano wa zaidi ya teknolojia moja na kwa lengo moja linalozingatia matakwa, kasi na viwango vya ubora.
Beadle, aliongeza kuwa kiuhalisia na kwa kuzingatia mahitaji ya soko nchini, Vodacom ndio kampuni pekee iliyojipanga kutoa huduma hiyo ya kasi kwa kuwa tayari. Hadi sasa imekwisha kamilisha awamu ya kwanza ya upitishaji wa huduma zake katika mkongo wa taifa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (NICTBB) pamoja na ule wa mawasiliano wa baharini unaopita sehemu kubwa duniani.

0 comments:
Post a Comment