SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, July 20, 2010

Rais Omar Al-Bashir kuelekea Chad licha ya waranti ya ICC iliyotolewa dhidi yake

Sample Image
Rais Omar Hassan Al-Bashir wa Sudan anatarajiwa kuelekea Chad hapo kesho ili kukutana na Rais Idris Deby wa nchi hiyo. Duru kutoka ofisi ya Rais Bashir zinasema kuwa kiongozi huyo atahudhuria mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Sahel Saharan na kwamba ziara hiyo itadumu kwa siku 3. Hii itakuwa safari ya kwanza ya Rais Bashir katika nchi mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ambayo mwaka uliopita ilitoa waranti ya kutiwa nguvuni kiongozi huyo kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita katika eneo la Darfur nchini Sudan. Baadhi ya washauri wake wamemtaka Rais Al-Bashair asiende Chad lakini kiongozi huyo amesema ana imani kuwa mwenyeji wake Rais Deby hawezi kumsaliti



Rais Kagame awahakikishia Wanyarwanda uchaguzi mkuu wa huru na wa haki

Sample ImageRais Paul Kagame wa Rwanda amewahakikishia Wanyarwanda kuwa uchaguzi mkuu wa rais utakaofanyika Agosti 9 utakuwa huru na wa haki. Akizungumza wakati wa kuzindua rasmi kampeni za uchaguzi, kiongozi huyo amesema kuwa wananchi watakuwa na fursa ya kuwachagua viongozi wanaowapenda bila kushinikizwa na mtu yeyote. Rais Kagame atatetea kiti chake kwa tiketi ya chama tawala cha RPF. Kagame amevikosoa vyama vya upinzani kwa kile alichokitaja ni mbinu chafu za kujaribu kulipaka tope jina zuri la chama chake.
Vyama vingine vya kisiasa bado vinakabiliwa na matatizo huku vingine vikiwa bado havijasajiliwa rasmi na hivyo kukifanya chama tawala kiendelee kupata nguvu.

0 comments:

Post a Comment