Mtu mmoja aliyekuwa amebeba mifuko yenye zaidi
ya maiti ya watoto wachanga 70 amekamatwa Nigeria.
Alikuwa ameajiriwa na chuo kikuu cha hospitali
inayotoa mafunzo ya afya mjini Lagos ya kupeleka maiti makaburini.
Inadaiwa mfanyakazi huyo alikuwa akijaribu
kutupa maiti hao kwani hakuwa na uwezo wa kulipa gharama za kuzikia.
Msemaji wa hospitali amesema wanashirikiana na
polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Mwandishi wa BBC mjini Lagos amesema familia
nyingi hazina uwezo kabisa wa kushughulikia maiti za watoto na wengine
hawana uwezo wa kulipia mahali pa kuhifadhia maiti, hivyo huwatelekeza
nje ya hospitali.
Hospitali hukodisha kampuni maalum kwa ajili ya
kuzika maiti hao.
'Aibu'
Afisa uhusiano wa polisi mjini Lagos Frank Mba,
alisema uchunguzi wa polisi wa awali pia ulisababisha kukamatwa kwa
baadhi ya wafanyakazi wa idara ya sayansi inayohusu viungo vya mwili
katika hospitali hiyo inayotoa pia mafunzo.
Amesema pia mshukiwa huyo hakuwa na nia ya
kutumia miili hiyo kwa matambiko.
Bw Mba alisema "Tuna uhakika mshukiwa huyo si
mtu anayefanya matambiko, si muuaji na wala si mtu anayeuza viungo.
Masuala mengine kama rushwa na utumiaji mbovu wa madaraka utachunguzwa."
Hospitali hiyo imeelezea tukio hilo kuwa ni la
aibu kwa shirika lililohusika.
Mwandishi wa BBC Fidelis Mbah alisema watu wengi
huko Lagos wameshtushwa na kutoamini kuwa hospitali hiyo yenye hadhi ya
kipekee ingeweza kuruhusu kampuni hiyo kushughulikia maiti za watu bila
usimamizi kutoka kwa wafanyakazi wake. bbc swahili
0 comments:
Post a Comment