Hispania yaiangamiza Ujerumani 1-0
Fainali ya Kombe la Dunia mwaka
2010 nchini Afrika Kusini itakuwa kati ya Hispania na Uholanzi.
Mpambano huo wa kihistoria umetokana na Hispania
kuishinda Ujerumani bao 1-0 katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban
na kufuzu fainali kwa mara ya kwanza katika historia.
Bao pekee la mechi hiyo lilifungwa kwa kichwa na
mlinzi Carles Puyol katika dakika ya 73, alipopanda mbele kucheza mpira
wa kona.
Ujerumani walionekana kikosi tofauti kabisa na timu
ambayo iliiondoa England kwa kuifunga mabao 4-1 na baadaye kuitandika
Argentina mabao 4-0 kwenye mechi ya robo fainali.
PWEZA ALIYETABIRI USHINDI WA SPAIN DHIDI YA GERMANY HUYU
PWEZA ALIYETABIRI USHINDI WA SPAIN DHIDI YA GERMANY HUYU
Uchochoro
Pengo la mshambuliaji Thomas Muller ambaye alikuwa
nje kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano lilikuwa wazi kabisa
kwenye safu ya ushambuliaji ya Ujerumani.
Muller ambaye ameshafunga mabao manne kwenye Kombe
la Dunia alipata kadi ya pili ya njano kwenye mechi kati ya Ujerumani na
Argentina, na bila yeye, kocha Joachim Loew alikosa kabisa mbinu za
ushambuliaji kwa timu ya Ujerumani.
Hispania walidhibiti mchezo katika muda wote, na
wangeweza kufunga mabao mengi zaidi lakini umaliziaji ukawa mbaya,
pamoja na mlinda lango wa Ujerumani, Manuel Nuer kuokoa mipira kadhaa.
Fainali ya siku ya Jumapili kati ya Hispania na
Uholanzi katika uwanja wa Soccer City mjini Johannesburg itawakutanisha
wafungaji wanaaongoza kwa sasa; Wesley Snijder na David Villa.
Ni mara ya kwanza kwa Hispania kucheza fainali ya
Kombe la Dunia, na kwa upande wa Uholanzi itakuwa mara ya tatu, ingawa
bado hawajapata kushinda Kombe hilo.
Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na wanne
itachezwa Jumamosi kati ya Uruguay na Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment