SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, July 7, 2010

Mayahudi waandamana kupinga mazungumzo ya Obama na Netanyahu mjini Washington
Sample Image 
Mamia ya Mayahudi wanaopinga Uzayuni wameandamana mjini Washington wakipinga mazungumzo ya 
Waziri Mkuu wa Utawala ghasibu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais Barack Obama wa Marekani. Katika maandamano hayo yaliyofanyika mbele ya ikulu ya Marekani White House, waandamanaji walibeba mabango yenye maandishi yanayokemea hatua za kiadui za utawala wa Israel dhidi ya sheria za Taurati. Wandamanaji hao wa Kiyahudi wamesema kuwa kuasisiwa utawala wa Israel katika ardhi za Palestina ni kinyume na dini na sheria za Kiyahudi.
Rais Barack Obama wa Marekani na Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel walikutana jana na kujadili suala la kuanzisha tena mazungumzo eti ya amani na Wapalestina. Obama amemhakikishia tena Netanhayu kwamba Marekani itaendela kulinda usalama na amani ya Israel na kuwa na uhusiano maalumu na dola hilo ghasibu. Kiongozi huyo wa Marekani pia amezitaka nchi za Kiarabu kujenga hali ya kuaminiana na utawala huo unaozikalia kwa mabavu ardhi tukufu za Palestina bila ya kuitaka Israel kusitisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi au kukomesha mauaji dhidi ya Wananchi wa Palestina. 
*****************************
Rais wa Nigeria asema migogoro ya kidini inatishia demokrasia 
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria
 Sample Image


ametahadharisha kuwa kutokuwepo hali ya kuvumiliana kidini ambako kumesababisha mauaji ya mamia ya watu nchini humo mwaka huu, kunatishia demokrasia. Rais wa Nigeria ambaye alikuwa akizungumza katika sherehe za Siku ya Kitaifa ya Jeshi amesema Wanigeria wanapaswa kutambua kwamba hatari kubwa inayotishia demokrasia na uhuru wao ni kosefu wa uvumilivu wa kidini na kikabila. Amesisitiza kuwa mashetani hao wanatishia nchi nzima ya Nigeria na umoja wake. Kiongozi huyo wa Nigeria alikuwa akiashiria mauaji yaliyotokea mwaka huu katika eneo la katikati mwa Nigeria.
Zaidi ya watu elfu kumi wameuawa katika machafuko na kidini na kikabila tangu kuanzishwa tena mfumo wa kidemokrasia nchini Nigeria mwaka 1999.
Jonathan amewataka askari wa Nigeria kujiepusha na jazba za kidini wakati wa kutekeleza majukumu yao.

0 comments:

Post a Comment