Ahmed Mohamed
Silanyo kiongozi wa chma cha upinzani cha eneo lililotangaza kujitenga
la Somaliland ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika
Juni 26. Essa Yusuf Mohammed mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya eneo hilo
ametangaza kwamba, Silanyo ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha
Kulmiye amepata asilimia 49.6 ya kura na kumshinda Rais Dahir Riyale
Kahin aliyepata asilimia 33.2 ya kura. Hii ni katika hali ambayo Faisal
Ali Warabe mgombea wa chama cha Haki na Uadilifu amepata asilimia 17.2
ya kura katika uchaguzi huo. Eneo linalojitawala la Jamhuri ya
Somaliland lililoko kaskazini mashariki mwa Somalia na ambalo ni koloni
la zamani la Uingereza, lilijitenga na Somalia mwaka 1991 lakini hadi
sasa halijatambuliwa kimataifa kuwa ni taifa huru. Pamoja na hayo
Somaliland inashuhudia amani ikilinganishwa na maeneo mengine ya
Somalia. |
0 comments:
Post a Comment