Kenya yaelezea wasi wasi wa kushambuliwa
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya
Moses Wetangula, ameonya kuwa wapiganaji wengi wa Kiislamu wanaingia
nchini Somali, kwa nia ya kufanya mashambulizi dhidi ya majirani wake,
ikiwemo Kenya.
Wetangula amesema kumekuwa na idadi kubwa ya
raia wa Afghanistan, Pakistan na kutoka nchi za Mashariki ya Kati
wanaoingia nchini Somalia.
Wetangula hata hivyo hajasema ni wapiganaji
wangapi wamefanikiwa kufika nchini humo, lakini amesema ni iadi yake ni
kubwa kiasi kwamba Kenya pamoja na jamii ya kimataifa imeanza kuwa na
wasi wasi.
Amesema hali hiyo inahitaji kushughulikiwa kwa
dharura.
Siku ya Jumatatu rais wa Somalia, Sheikh Sharif
Sheikh Ahmed, alionya kuwa taifa hilo lina thibitiwa na kundi la kigadi
la Al-Qaeda na makundi mengine ya wapiganaji wa Kiislamu.
******************************
Matatizo ya moyo huenda yalisababisha kifo cha
Chebeya
Kundi la wachunguzi wa
kimatibabu wa kimataifa wanaochunguza chanzo cha kifo cha mwanaharakati
wa kutetea haki za kibinadam nchini jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
wamesema hawajafanikiwa kutambua kile kilichosababisha kifo hicho.
Wachunguzi hao wanasema kifo hicho huenda
kilisababisha na matatizo ya moyo.
Mwili wa Floribert Chebeya, ulipatikana ndani ya
gari lake huku mikono yake ikiwa imefungwa, siku moja tu baada ya
kuamriwa kufika mbele ya afisa mkuu wa polisi nchini humo, John Numbi.
Chabeya alifahamika kutokana na juhudi zake za
kupinga mauaji ya kiholela nchini Congo.
Kifo chake kilisababisha raia wa nchi hiyo na
wanaharakati wa kuetetea haki za kibinadamn kuitisha uchunguzi wa
kimataifa.
Ilifahamika wazi kuwa Bw. Chabeya alikuwa na
matatizo ya moyo kwa muda mrefu.
Madaktari kutoka Uholansi kwa ushirikiano na
wenzao kutoka Congo walifanya uchunguzi huo.
bbc swahili.
0 comments:
Post a Comment