Kinyan'ganyiro cha mshindi 3
Ujerumani yaumana kesho na
Uruguay,Paul asemaje ?
Pweza "Paul" alipoagua ushindi wa Spain dhidi ya Ujerumani.
PWEZA PAULO ATABIRI MATOKEO YA FAINALI KOMBE LA DUNIA?
"Paul"-Pweza kutoka Oberhausen, Ujerumani, aliegonga vichwa vya habari duniani kwa kuagua sawa sawa : ni timu gani itashinda, anatazamiwa hivi punde kutoa utabiri wake ni timu gani itaibuka bingwa wa dunia hapo Jumapili kati ya Spain na Holland. Na tangu Holland hata Spain, wanasubiri kwa hamu "Paul" atasema nini leo.Mashabiki wa Ujerumani hawajali tena vipi Paul anaagua leo mpambano wa kesho wa kuania mshindi wa 3 kati yao na Uruguay utakavyomalizika huko Port Elizabeth. Hata hivyo, mpambano huo unaahidi msisimko mkubwa, kwani Wauruguay, mabingwa wa kwanza wa dunia , wanataka kuthibitisha kwamba hatua walizopiga katika kombe hili la dunia haikuwa bahati nasibu tu.

Ujerumani na Uruguay , zimeshapambana mara 3 katika kombe la dunia na
matokeo ya hadi sasa, yameonesha Wauru wanapokutana na Wajerumani, kila
mara wanazidi nguvu.
Mpambano wa mshindi watatu huko Port Elizabeth , unaoitwa
"finali-ndogo" ya Kombe la dunia , alao kwa Uruguay, utakuwa ni kilele
cha dimba lao baada ya Kombe la dunia lililowasangaza mashabiki wengi
ulimwenguni kwa matokeo iliopata Uruguay huko Afrika kusini.
Endapo Uruguay, ikiishinda Ujerumani , mabingwa hawa marambili wa
dunia (1930 na 1950), watakuwa wamefika mbali kabisa tangu kupita miaka
40. Kwani, 1954 na 1970 Uruguay, ilimalizia nusu-finali.
Ujerumani, haitataka chochote kasoro ya ushindi hapo kesho ili
kukamilisha Kombe hili la dunia kwa ufanisi. Bila ya ushindi , Kombe la
dunia mwaka 2010 licha ya kusifiwa mno na ushabiki mkubwa wa wapambe
wake, litakuwa pigo kwa Ujerumani baada ya kumaliza makamo-bingwa 2002
huko Korea ya kusini na Japan na nafasi ya 3 nyumbani, Ujerumani mwaka
2006.
Changamoto ya kwanza kabisa kati ya Ujerumani na Uruguay, ilikuwa
Julai 23, 1966 huko Shefield, Uingereza, pale timu hizi mbili
zilipochuana katika robo-finali. Ujerumani ikashinda kwa mabao 4:0.
Timu hizi mbili zikakumbana tena katika Kombe la dunia, 1970 huko
Mexico kuania mshindi watatu kama hapo kesho. Kinyume na changamoto ya
1966, mpambano huu ulimalizikia ushindi wa bao 1:0 wa Ujerumani.
Ujerumani na Uruguay, zikakutana tena kwa mara ya tatu katika Kombe
la dunia huko huko Mexico,1986. Mara hii Uruguay, ilizima vishindo vya
Ujerumani katika duru ya kwanza na kugawana pointi zilipoachana sare bao
1:1.
Bingwa wa dunia 1990, stadi wa Ujerumani, Andreas Brehme, amesema
kuwa, mshangao mkubwa wa Kombe hili la dunia, 2010 , ni kufika mbali
sana kwa Uruguay. Hakuna bingwa yoyote wa dimba huko Amerika kusini
kwenye wazimu wa dimba, alieweza kubashiri hayo. Kwani katika kundi lao,
timu zilizopigiwa upatu kutamba ni makamo-bingwa wa dunia-Ufaransa na
Mexico. Hata wenyeji, Bafana Bafana, waliokuwa pia kundi hili,
walitazamiwa kuwapiku Wauruguay.
Mwishoe, Uruguay iliparamia kileleni mwa kundi lake katika duru ya
kwanza na shukurani kwa mkono wa Suarez, katika lango lao walipocheza na
Ghana, Uruguay, imefika umbali wa kucheza mpambano wa mshindi watatu na
Ujerumani kesho.
Iliosalia sasa ni kusubiri kuona hivi punde, nini "Paul", pweza wa
Oberhausen, ameagua juu ya hatima ya Ujerumani mara hii na ile ya Spain
na Holland keshokutwa. Mashabiki wa pweza huyu maarufu-mtabiri mpya wa
dimba, wanadai "msiandikie mate na Paulo yupo."
Mwandishi: Martinez,Daniel (DW)
0 comments:
Post a Comment