Mh.
Mengi na Charles Hillary wakutana Sauzi
*****************************
Mkutano
wa Kamati Kuu ya CCM Dodoma
Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba akimkaribisha
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa
White House tayari kuongoza kikao cha kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo
asubuhi.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi.Wengine
waliokaa meza kuu kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin
Mkapa, Rais Mstaafu awamu ya Pili ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Amani Abeid Karume,Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba, makamau mwenyekiti
wa CCM Bara Pius Msekwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar Salmin Amour.
Wagombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Makamu wa
Rais Dr.Ali Mohamed Shein na Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha
wakisalimiana katika viwanja vya makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo
asubuhi.
Mgombea Urais wa Zanzibar ambaye pia ni Waziri kiongozi
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha akisalimia
baadhi ya wanachama wa CCM mjini Dodoma muda mfupi kabla ya kuanza kikao
cha Kamati kuu ya CCM.
Mgombea urais wa Zanzibar Balozi Ali Karume akisalimia
baadhi ya wanachama wa CCM mjini Dodoma leo asubuhi.(picha na Freddy
Maro) 



0 comments:
Post a Comment