SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, July 24, 2010


Happiness Mwanafunzi Bora Katika Shule 150 Duniani
Babu yake na Happiness Watimanywa mzee Shem Kalenga, mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Tabora Jazz, akimpongeza mjukuu wake katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika kwenye hoteli ya Lamada.
Mtoto Happiness wa pili kushoto akiwa katika picha na wazazi wake na wadogo zake katika sherehe ya kumpongeza iliyofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya Lamada.
Mkurugenzi wa ukaguzi wa shule za sekondari nchini na kaima kamishna Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Mama Wasena akitoa hotuba ya kumpongeza mtoto Happiness Watimanywa kwa kufanya vizuri katika mitihani yake ambapo mtoto huyo ameongoza katika shule 150 duniani za mtandao wa IGCSE. Happiness alikuwa akisoma katika shule ya Saint Constantines International School ya Arusha.
Kaimu Kamishna Mama Wasena amempongeza mtoto huyo na kumpa sifa nyingi lakini pia amesifu kwa kuwa ameiletea sifa Tanzania na Wizara ya Elimu kwa ujumla jambo ambalo lilithibitishwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Mwatumu Mahiza ambaye alimpongeza mtoto huyo wakati alipokuwa kiwasilisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka huu wa fedha. Picha na John Bukuku

0 comments:

Post a Comment