SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, July 20, 2010


Ahmadinejad: Wamagharibi wanaogopeshwa na mwamko wa Iran

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba licha ya nchi za Magharibi kuweka vikwazo vingi dhidi ya Tehran, lakini bado zina wasiwasi kutokana na kuongezeka mwamko wa taifa la Iran.Amesema hayo katika sherehe za kufungua mradi mkubwa wa kiviwanda huko Qazvin, magharibi mwa mji mkuu wa Iran na kuongeza kuwa, madola ya Magharibi hayana wasiwasi na silaha za atomiki, bali kinachowatia woga ni mwamko wa taifa la Iran.Amesisitiza pia kuwa, lengo la nchi za Magharibi la kuiwekea vikwazo hivi na vile Iran ni kutaka kuona taifa hili linajidhalilisha kwa madola ya kibeberu lakini amesema hilo halitatokea kamwe na daima vijana wa Iran wataendelea kufikia vilele mbali mbali vya ustawi na maendeleo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.Vile vile amevilaumu vikosi vya NATO vilivyoko Afghanistan na vile ya Marekani vilivyoko Pakistan kwa kuyasaidia makundi ya kigaidi kufanya vitendo vya kigaidi ndani ya Iran kama vile miripuko miwili ya bomu iliyotokea kwenye msikiti mkuu wa Zahedan huko kusini-mashariki mwa Iran hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment