Viongozi wa
Zimbabwe wameanzisha kampeni mpya ya kutafuta maoni ya wananchi kuhusu
katiba mpya huku uchaguzi mwingine ukipangwa kufanyika mwakani.
Rais Robert Mugabe na adui yake wa zamani Morgan Tsvangirai ambaye sasa ni Waziri Mkuu wa Zimbabwe, wamewataka wananchi wa nchi hiyo kuwa watulivu na kujiepusha na vitendo vya machafuko.
Morgan Tsvangirai amedai kuwa alikubali kuingia serikalini kwa sharti kwamba kupatikane katiba mpya itakayochukua nafasi ya ile ya mwaka 1979 ambayo ilitungwa kabla ya Zimbabwe kupata uhuru wake kutoka kwa mkoloni mkongwe wa Ulaya yaani Uingereza.Amedai kuwa, katiba hiyo mpya ilibidi ibuniwe tangu miezi minane iliyopita.
Miongoni mwa vipengee ambavyo Rais Robert Mugabe hataki vibadilishwe katika katiba ya sasa ni kile kinachompa haki Rais, ya kugombea kwa vipindi vyovyote anavyotaka.
Tsvangirai ana uungaji mkono mkubwa wa madola ya kikoloni na kibeberu ya Magharibi ambayo yalikasirishwa sana na hatua ya Mugabe ya kutwaa baadhi ya mashamba yaliyokuwa yamehodhiwa na walowezi wachache wa Kizungu na kuwapa wazalendo wa Zimbabwe.

Msafara nambari mbili wa uhuru kuelekea Ghaza mwezi ujao |
Wanaharakati
wa haki za binaadamu barani Ulaya wanapanga kutuma msafara mwingine wa
meli zenye misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya wananchi madhlumu wa
Ghaza mwezi ujao wa Julai.
Hilo litakuwa ni jaribio jingine la kuvunja mzingiro wa Ghaza uliowekwa na utawala dhalimu wa Kizayuni. Kampeni ya Kukomesha Mzingiro wa Ghaza ya Barani Ulaya imesema kwamba tayari kuna meli sita zilizo tayari kuelekea Ghaza. Hayo yamekuja katika hali ambayo Bunge la Ulaya limekwama kwenye mijadala kuhusu namna ya kuamiliana na mashambulizi ya kikatili yaliyofanywa na makomandoo wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Msafara wa Uhuru uliokuwa na meli sita zenye misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya wananchi wa Ghaza. Tarehe 31 mwezi uliopita wa Mei, utawala wa Kizayuni uliuvamia msafara huo uliokuwa na wanaharakati kutoka nchi 42 duniani, shambulizi la kikatili ambalo lilipelekea makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa. |
0 comments:
Post a Comment