Zenani Mandela, mwenye umri wa miaka 13,
alifariki dunia baada ya kutoka kwenye tamasha la Kombe la Dunia mjini
Soweto.
Kufuatia msiba huo, Bw Mandela aliahirisha
mipango yake ya kuhudhuria ufunguzi wa shindano la Kombe la Dunia.
Dereva wa gari hilo, ambaye ni rafiki wa karibu
na familia ya Mandela, alikamatwa na mwanzo kushtakiwa kwa kuendesha
akiwa amekunywa pombe, lakini hajafikishwa mahakamani mpaka baada ya
Kombe la Dunia kumalizika.
Shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi Bw Mandela,
mwenye umri wa miaka 91, alifanya kampeni ili Kombe la Dunia lifanyike
Afrika Kusini.
Taswira kupitia televisheni zimemwonyesha
akiinuka huku akisaidiwa na mke wake Graca Machel alipokuwa akielekea
kwenye benchi la mbele la kanisa dogo lililopo kwenye shule ya Zenani
mjini Johannesburg, ambapo msiba huo unapofanyika.
Aliyekuwa mke wa Mandela, Winnie
Madikizela-Mandela mama mzazi wa mama yake wa Zenani naye pia alikuwepo,
pamoja na viongozi maarufu kwenye nyanja za kisiasa, burudani na
michezo na baadhi ya waliosoma nao Zenani.
Kwaya ya nyimbo za injili ya Soweto iliimba
wakati wageni walipowasili, baadae wimbo wa miondoko ya Soul ya Bill
Wither, Lean on Me ilichezwa huku picha za Zenani zikionyeshwa kwenye
skirini.
Shughuli hiyo inatarajiwa kufuatiwa na maziko ya
watu wachache.
Zenani alisherehekea siku yake ya kuzaliwa
alipotimiza miaka 13 tarehe 9 Juni. Alikuwa miongoni mwa vitukuu tisa wa
Bw Mandela.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye rekodi mbaya
sana ya usalama wa barabarani, na kuna takriban vifo vya watu 42 kila
siku katika barabara ya nchi hizo.
Tamasha la Kombe la Dunia la siku ya Alhamis
liliwavutia maelfu ya watu katika uwanja wa Orlando mjini Soweto, huku
kukiwa na msongamano mkubwa wa magari mapema Ijumaa.
Tamasha hilo liliwajumuisha wasanii nyota wa
kimataifa, akiwemo mwimbaji wa Colombia Shakira, Black Eyed Peas na
Alicia Keys, pamoja na wasanii maarufu wa Afrika Amadou & Mariam na
Hugh Masekela.
0 comments:
Post a Comment