Wakati shirika la umoja wa mataifa la kuwashughulikia wakimbizi
likitangaza
kiwango kidogo zaidi duniani cha kurudi makwao wakimbizi kuwa
kushuhudiwa katikamuda wa miongo miwili ,visa vinavyothibitisha jinsi
ilivyo
vigumu kwa wakimbizi kurudi makwao ni vile vya nchi hiyo ya Burundi.
Kwa maelfu ya wakimbizi wa Burundi walioikimbilia nchi jirani ya
Tanzania
katika miaka ya 70,baada ya miongo minne sasa wamekuwa raia wa
Tanzania.
Hii ni baada ya hatua iliyotangazwa na serikali ya Tanzania mwezi
Aprili
mwaka huu kuwahalalisha Warundi takriban 162,000 na familia zao kuwa
Watanzania.
Wengi wa wakimbizi hao waliokuwa wakiishi katika kambi tatu kubwa
magharibi mwa Tanzania walikuwa wamekosa matumaini ya kuwa raia na
kudhani kuwa wengi wao wangekufa wakiwa bado wakimbizi.
Wiki chache zilizopita, Ferederiko Kivulunzi mwenye umri wa miaka 59
ana
ambaye aliwasili Tanzania akiwa na miaka 21 1972 alipoyakimbia machafuko
kwao Burundi anasema" sasa wameondokana na ile hali ya kuitwa wakimbizi
na kuweza kujivuna kwamba sasa ni Watanzania. Anasema sasa wanaweza
kutembea wakiwa huru kama Mtanzania mwengine yeyote."
Sasa furaha inaonekana miongoni mwao kufuatia uamuzi huo ambao pia
unawaruhusu kuzunguka huru kinyume na ilivyokuwa walipokuwa kambini
kama wakimbizi.
Hata hivyo hali ni tofauti nchini Burundi ambapo maisha ya wakimbizi
takriban
nusu milioni walioamua kurudi nchini humo yangali duni.
Nyumba mojawapo kwa wakimbizi wa Burundi wanaorudi nyumbani.
wengi wao wanakosa ardhi za kuishi,baada ya ardhi zao kunyakuliwa na
waliokuwa majirani zao ama kutokana na miradi iliyoanzishwa na serikali
katika ardhi hizo.
Wengi wa wakimbizi hawa wameamua kupata hifadhi katika kijiji kimoja
kinachofahamika kama 'kijiji cha amani'kilicho jengwa na shirika la
Umoja wa
Mataifa linalowashughulikia wakimbizi kwa minajili ya kuwahifadhi maelfu
ya
Wahutu wanaorudi nchni humo na Watutsi walioachwa bila makaazi nchini
humo ambao serikali haijui iwafanyeje.
Sambamba na nyumba ndogo, wanaorudi n yumbani hupewa mbuzi watatu
na mipapai na mipera iliokwisha oteshawa. Mkimbizi mmoja kawa jina la
Saphia anaishi mtaa watatu wa wa eneo hilo la makaazi, nyumba nambari
125, anasema anashukuru kwa kupatiwa nyumba lakini analalamika kwamba
waliorudi nyumbani na kupewa makaazi katika kijiji hicho cha amani
hawana
njia ya kukidhi mahitaji yao kimaisha kwa sababu hawana ardhi. Wote
wanategemea vibarua vya kubahatisha ambapo malipo ya kazi ni mabaya
mno.
Naye Densis Niyungeko anayeishi nyumba nambari 238 katika mtaa wa
sita,
alizaliwa Congo iliokuwa zamani Zaire baada ya wazazi wake Warundi
kukimbilia huko 1972. Yeye pia aakaikimbia Congo wakati wa vita vya
1996-97 kwanza akikimbilia Tanzania na baadae kurudi nymbani kwa asili
Burundi.
na ingawa hufafadhahika baadhi ya wakati kwa ukosefu wa ajira ya kudumu
na kutegemea kibarua cha reja reja, hata hivyo anasema anafuraha kurudi
nyumbani. aanamalizia kwa usemi, uhamishoni ni uhamishoni tu- mtu Kwao !
Mwandishi: Maryam Dodo Abdalla/AFP
0 comments:
Post a Comment