SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 20, 2010

Waziri Mkuu wa Ethiopia aikosoa vikali Ethiopia kuhusiana na maji ya Mto Nile

Thursday, 20 May 2010 Sample ImageMeles Zenawi Waziri Mkuu wa Ethiopia ameikosoa vikali serikali ya Misri kutokana na kung'ang'ania msimamo wake wa awali kuhusiana na umiliki wa maji ya mto Nile. Zenawi ameongeza kuwa, serikali ya Misri haiwezi kuizuia Ethiopia kujenga mabwawa yatakayohifadhi maji yanayotoka Mto Nile. Zenawi ameongeza kuwa, baadhi ya watu nchini Misri wanafikiri kwamba maji ya Mto Nile ni milki ya nchi hiyo, na serikali ya Cairo ina haki ya kuchukua uamuzi wowote kuhusiana na mgawo wa maji hayo. Ameongeza kuwa, baadhi ya Wamisri wanaamini kwamba nchi ambazo ni chimbuko la mto Nile, haziwezi kutumia maji hayo kwa vile ni masikini na hazina uthabiti. Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa, licha ya kuwa Ethiopia ni nchi masikini lakini inaweza kutumia mali asili zake kwa ajili ya kuimarisha uchumi na miundo mbinu yake. Nchi nyingine zinazopakana na maji ya mto Nile zinataka yawepo makubaliano mapya ambayo yatakuwa na mgawanyo sawa katika utumiaji wa maji ya mto huo mrefu zaidi barani Afrika.
Radio Swahili.

0 comments:

Post a Comment