Akina mama watatu wa Kimarekani ambao watoto wao wametiwa mbaroni baada ya kuingia nchini Iran kinyume cha sheria, wameiomba serikali ya Marekani iwaruhusu akina mama wa Kiirani waonane na watoto wao ambao wanashikiliwa nchini humo. Sarah Shourd, Shane Bauer na Josh Fattal walitiwa mbaroni mwezi Julai mwaka jana na kikosi cha usalama cha Iran baada ya kuingia kinyume cha sheria kwenye ardhi ya Iran wakitokea kaskazini mwa Iraq. Akina mama hao walionyesha furaha zao walipokutana na watoto wao, na kuishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na muamala mzuri waliouonyesha kwa watoto wao. Wakati huohuo, Haidar Muslihi Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran amesema kuwa, raia hao watatu wa Marekani wanaoshikiliwa nchini wanakabiliwa na tuhuma za kufanya ujasusi nchini. |
Thursday, May 20, 2010
Wamarekani waridhishwa na hali za watoto wao wanaotuhumiwa kwa ugaidi
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, May 20, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment