Rais Barack Obama amefurahishwa na makubaliano yaliyoafikiwa
katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa, kuhusiana na mkataba wa kuzuia
kusambaa kwa silaha za nyuklia. Hata hivyo Obama alipinga vikali, kile
alichokitaja ni kuilenga Israel, katika mkutano uliopangwa kufanyika
mwaka 2012, na kuyaleta pamoja mataifa yote ya Mashariki ya Kati, ili
kuondolea mbali kitisho cha silaha za nyuklia katika Mashariki ya Kati.
Mataifa matano yanayomiliki silaha za Nyuklia, na ambayo yametia saini
mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha hizo, yalikubaliana kuchukua
hatua zaidi kuzuia tishio la silaha za nyuklia duniani. Mataifa hayo
yanayoongozwa na Marekani, Urusi, China, Ufaransa na Uingereza- yote
yameridhia pendekezo la kupunguza zana zao za nyuklia. Hatua hii sasa
inaiwekea mbinyo zaidi Israel, pamoja na India, Pakistan na Korea
Kaskazini- mataifa matatu ambayo yamekataa kutia saini mkataba huo wa
kusambaa kwa silaha za nyuklia.
Watu wenye silaha washambulia misikiti na kuua watu 80 Lahore
Habari kutoka
Pakistan zinasema kuwa watu wenye silaha wamewavamia waumini wa Kiislamu
katika msikiti mmoja mjini Lahore Pakistan na kuwaua watu wasiopungua
80. Inaripotiwa kuwa mamia ya watu pia wanazuiliwa mateka na genge hilo.
Duru za habari zinasema kuwa shambulio hilo limetokea mapema leo wakati
wa swala ya Ijumaa katika misikiti kadhaa mjini Lahore. Inasemekana
kuwa magaidi hao walitumia maguruneti pamoja na silaha zingine hatari
kutekeleza shambulio hilo. Polisi imeanzisha uchunguzi ili kuwakamata
waliohusika.
|
0 comments:
Post a Comment