SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 26, 2010

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuondoka Chad

NEW YORK
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuwaondoa wanajeshi wa kulinda amani wa umoja huo kutoka Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati kufuatia shinikizo la serikali ya Chad. Wanajeshi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINURCAT, watapunguzwa kutoka 3,300 hadi 2,200 ifikapo Julai 15 mwaka huu. Watakaobakia wataondoka maeneo hayo ifikapo Desemba 31 mwaka huu.
Serikali ya Chad ililalamika kwamba vikosi vya kimataifa haviwezi kuwalinda raia na ikaamua kuchukua jukumu hilo kwa kuutaka Umoja wa Mataifa uwaondoe wanajeshi wake. Maafisa wa umoja huo wana wasiwasi hali ya wakimbizi huenda ikazidi kuwa mbaya mara tu wanajeshi hao watakapoondoka. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema wanajeshi kadhaa watabakia ili kuisadia Chad.
Deutsche Welle

0 comments:

Post a Comment