Ripoti iliyotolewa na baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa imesema makundi ya waasi mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanaendelea kukusanya ushuru kinyume
cha sheria kutoka kwa watu wanaohudumu katika kiwanda cha kuchimba
madini ya dhahabu.
Ripoti hiyo pia imewasilisha ushahidi
kuthibitisha kuwa waasi hao wanatumia stakabadhi gushi za Umoja huo ili
kuyauza madini hayo katika mataifa jirani.Waasi wa CNDP vile vile wametuhumiwa kuweka vituo vya ukaguzi na kuwatoza wenye magari na raia kodi kinyume cha sheria.
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ina mali asili za madini nyingi lakini makundi ya waasi wenye silaha wanadhibiti biashara hii.
Makundi haya yanaarifiwa kupata faida kutokana na biashara hii ya mamilioni ya dola kutokana na madini na kudhibiti migodi kwa nguvu na kuomba hongo au kodi.
Mchango wa biashara ya madini umetambulika kuwa moja ya sababu zinazochochea vita na kuchangia ukiukwaji wa haki za binadamu mashariki mwa nchi hii tangu kuanza kwa vita.
0 comments:
Post a Comment