Maafisa wa shughuli ya uokoaji
nchini Uganda wanasema wanajitahidi kufukua mamia ya miili ya watu
waliozikwa hai kufuatia maporomoko ya ardhi katika wilaya ya Bududa
miezi mitatu iliyopita.
Kwa mujibu wa ripoti ya serikali zaidi ya watu
mia mbili hawajulikani waliko, huku miili mia moja ikiwa imefukuliwa.Kiongozi wa shughuli hiyo Luteni Kanali Wilson Kabera, amedokeza shughuli hiyo imetatizika kutokana na mvua kubwa na pia matatizo ya kuharibika kwa mitambo na mashini zinazotumika kufukua miili hiyo.
Zaidi ya watu elfu nane walihama makwao kutokana na maporomoka hayo ya ardhi.
0 comments:
Post a Comment