Serikali ya Marekani imetoa onyo
kwa raia wake kuwa Afrika Kusini inakabiliwa na tishio la ugaidi wakati
wa Kombe la Dunia.
Imesema matukio yanayoshughulisha umati mkubwa
wa watu huwavutia magaidi kufanya mashambulio.Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema, " Kuna hatari kubwa kuwa makundi ya wapiganaji yanaweza kufanya ugaidi ndani ya Afrika Kusini siku za usoni."
Onyo hilo limetolewa wakati Rais Barack Obama akiitakia kheri timu ya soka ya Marekani.
Bw Obama, aliyeambatana na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bill Clinton aliwaaga wachezaji hao kwenye ikulu ya White House, " Nataka tu kusema jinsi gani tunavyosikia fahari juu ya timu hiyo."
Amesema, " Kila mmoja atakuwa anawashangilia."
"Na japokuwa mara nyingi hatukumbuki hilo hapa Marekani, hili litakuwa shindano kubwa zaidi la soka duniani."
Katika taarifa iliyotolewa, wizara ya mambo ya nje imesema haina taarifa kamili ya vitisho wakati wa mashindano hayo, lakini vitisho vimeripotiwa na vyombo vya habari.
Afrika Kusini imeandaa maelfu ya polisi waliopitia mafunzo maalum kushughulika na usalama wa mashabiki.
Takriban watu 350, 000 wanatarajiwa kutembelea Afrika Kusini kwa ajili ya Kombe la Dunia, linalofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na kuanza Juni 11.
0 comments:
Post a Comment