Mshauri wa
masuala ya kisiasa wa Rais Omar al Bashir wa Sudan amekanusha madai
kwamba kiongozi wa chama cha upinzani cha Congresi ya Taifa Dakta Hassan
Turabi ametiwa nguvuni kutokana na madai yake juu ya kufanyika
udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa mwezi uliopita nchini humo. Mustafa
Othman Ismail amesema Turabi amekatwa kutokana na kuchapicha taarifa
zinazotishia usalama wa taifa wa Sudan katika gazeti la chama chake.
Amesema kuwa sheria za magazeti za Sudan zinamtwisha Mhariri Mkuu na Mwenyekiti wa chama kinachomiliki gazeti husika hatia au lawama za ripoti za uongo zinazochapishwa katika gazeti hilo. Mshauri wa masuala ya kisiasa wa Rais wa Sudan amesema gazeti la chama cha Congresi ya Taifa lilichapisha ripoti isiyokuwa sahihi likidai kuwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran liko mjini Khartoum na kwamba linatengeneza silaha za kisasa kwa ajili ya serikali ya Sudan na nyingine zinapelekwa kwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas huko katika Ukanda wa Gaza.
Bwana Ismail amesema Turabi atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayohusiana na madai hayo yanayohatarisha usalama wa taifa.
Vyombo vya usalama vya serikali ya Sudan vilimtia nguvuni Hassan Turabi Jumamosi iliyopita bila ya kutoa maelezo yoyote.

Kiswahili Radio
0 comments:
Post a Comment