SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 14, 2010

Sean Kingston kufanya maajabu


MSANII maarufu nchini Marekani, Sean Kingston amewasili nchini juzi kwa ajili ya kufanya onyesho katika sherehe za kuwapongeza washindi wa Kili Music Awards kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Tuzo za kili Music Awards zinafanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa wasanii mbalimbali kupewa tuzo  na kesho atajumbuika na wasanii hao kufanya shoo.
Akizungumza na Wanahabari katika Hotel ya Double tree iliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam alisema kuwa amefurahi sana kuja Tanzania kwa ajili ya kuinua muziki wa hapa kwani atakuwa moja ya watu ambao watatoa tuzo hizo ambayo ni msanii atakayeshinda Wimbo bora wa RAGA.
Alisema kuwa kwa mara ya kwanza amekuja Tanzania, lakini amevutiwa sana na Tanzania pia, amependa utamaduni wa Tanzania .
Alisema mbali na kutoa tuzo hiyo msanii huyo atatumbuiza Jumamosi akiwa pamoja na wasanii ambao wameshinda tuzo za Kili na amehaidi kufanya maajabu katika shoo zake hapo kesho.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa msanii huyo atafanya  ziara mbali mbali katika  na jana alikutana na wasanii wanaowania tuzo hizo kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya kimuziki.
Alisema anaamiki kuwa msanii huyo atafurahia Tanzania na kurudi tena kama baadhi ya wasanii kutoka Marekani waliowai kuja ni Jay  Z, 50Cent, Ja Rule na Busta rymes, Joe Tomas, Eve, Fat Joe.

0 comments:

Post a Comment