SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 14, 2010

Uswisi yarejesha kinyago kilichoibwa Tanzania

Patricia Kimelemeta
SERIKALI imepokea kinyago cha kimakonde kilichopotea katika jumba la makumbusho zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Kinyago hicho, kilihifadhiwa katika jumba hilo kwa ajili ya kufanya maonyesho kwa wageni waliokuwa wakitembelea maeneo hayo na baadhi ya watu walikiiba na kukiuza kwenye mnada.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Maliasili na Utalii , Shamsa Mwangunga alisema kinyago hicho, kilinunuliwa na raia ya Uswis ambaye alikihifadhi  kwenye makumbusho yao ya Taifa.
 “Kinyago hiki kilipotea muda mrefu, lakini ushirikiano uliopo baina yetu na Interpol tumeweza kufanikiwa kukipata, kutokana na hali hiyo tutaendelea kulinda mali zetu ili kuhakikisha haiziibiwi,”alisema Mwangunga.
Alilisema kutokana na hali hiyo, serikali ya Uswis ilitoa ushirikiano na kurudisha kinyago hicho baada ya kubaini kuwa ni cha wizi, jambo ambalo liliwafanya wakitoe kwenye maonyesho yao.
Mwangunga alisema serikali itaendelea kutafuta mali zilizopotea katika nchi nyingine ili wazirudishe na kuzihifadhi kwenye makumbusho kwa ajili ya kuwaonyesha wageni.
Alisema kutokana na hali hiyo, serikali pia itaendelea kulinda mali zilizopo ili kudhibiti wizi wa aina hiyo.
Mwangunga alisema mchakato uliopo ni kuhakikisha mali hizo, zinaingiza pato la Taifa kwa aina moja au nyingine.

0 comments:

Post a Comment