Na Elizabeth Mayemba
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa sasa yupo huru kwenda kuichezea
timu ya Azam FC msimu ujao, baada ya kikao cha viongozi wa pande zote
mbili kukubaliana mambo mbalimbali.
Kikao cha kujadili ofa ya mchezaji huyo kilianza juzi na jana
mchana, kilimalizika ambapo Azam FC, walianza utaratibu wa kuwalipa
Yanga dola za Marekani milioni 40 (zaidi ya sh.milioni 50 za Tanzania).
Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zinadai kuwa, kikubwa kilichokuwa
kinajadiliwa katika kikao hicho ni dau la mchezaji huyo, ambapo
walikubaliana kutoa kiasi hicho cha fedha na kutoa baraka kwa mchezaji
huyo kutua Azam.
"Sasa hivi (jana) tunakwenda kuchukua kiasi hicho cha fedha ili
tumalizane na wenzetu wa Yanga, kikao kilikuwa cha amani na tulifuata
taratibu zote zinazotakiwa," kilidai chanzo hicho cha Azam kutoka ndani
ya kikao hicho.
Chanzo hicho kilidai kuwa, baada ya kukamilisha mipango ya kumnasa
Ngassa, sasa wanaendelea na mipango mingine ya kutafuta wachezaji
wengine kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao msimu ujao.
Kilidai kuwa, msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamepanga kunyakua
ubingwa wa Bara, ili nao waweze kushiriki michuano ya kimataifa.
Pia, klabu ya Yanga inaweza kumpoteza beki wake mahiri Nadir Haroub
'Cannavaro' ambaye naye anadaiwa kutaka kuhamia klabu hiyo ya Azam FC.
Majira.
Saturday, May 22, 2010
Ngassa njia nyeupe Azam
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Saturday, May 22, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment