Maaskofu wa
Makanisa ya Ubelgiji leo wameomba msamaha kwa wahanga wote wa vitendo
vya udhalilishaji wa kijinsia walivyofanyiwa na baadhi ya maaskofu
kutokanchi mbalimbali duniani. Taarifa iliyotolewa na maaskofu hao
imeeleza kuwa, wanawaomba radhi wahanga wote ambao walidhalilishwa
kijinsia hivi karibuni na kundi la maaskofu waliopotoka katikanchi
mbalimbali ulimwenguni. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, jukumu kubwa la
maaskofu ni kudhamini usalama wa watoto, na kutaka tabaka hilo la watoto
lihifadhiwe duniani kote. Baada ya kufichuliwa kashfa ya Maaskofu huko
Austria, Ujerumani, Ireland na Marekani ya kuwanajisi watoto wa nchi
hizo, Kanisa la Ubelgiji mwezi uliopita lilitaka maaskofu wote
waliokumbwa na kukiri kutenda vitendo hivyo vichafu wanga'atuke katika
uongozi wa kidini. Miaka 25 iliyopita Askofu mmoja wa mji wa Bruges
alikuwa ni askofu wa kwanza wa Kikatoliki nchini Ubelgiji kuamua kujitoa
kwenye uongozi wa kiroho baada ya kukumbwa na kashfa ya kuwanajisi
watoto. Kiswahili Radio. |
Thursday, May 20, 2010
Maaskofu wa Ubelgiji waomba msamaha kwa wahanga walionajisiwa
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, May 20, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment