Misururu mirefu ya wapiga kura ilionekana kwenye vituo vya kupigia kura katika mji mkuu, Addis Ababa, kabla ya vituo kufunguliwa.
Waziri mkuu Meles Zenawi, washirika wa karibu wa nchi za magharibi ambao hupambana dhidi ya wapiganaji wa Somalia, wanapigania kuchaguliwa tena.
Lakini upinzani umeshaanza kulalamika juu ya uchaguzi huo.
Msemaji wa muungano wa upinzani, Medrek, amesema waangalizi wake wamekuwa wakitishiwa na kukamatwa katika baadhi ya maeneo nchini humo.
Nagesso Gidada ameliambia shirika la habari la AP, "Tunadhani hatutakubaliana na matokeo.
" Msemaji wa serikali amepuuza madai hayo, akisema upinzani lazima ukubali kushindwa.
Mwandishi wa BBC Will Ross aliyopo Addis Ababa amesema vituo vya kupigia kura alivyotembelea kwenye mji mkuu vilikuwa na mpangilio mzuri, na wapiga kura wakijitokeza wa kutosha.
Upinzani umedai kulifanyika hila wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005 ili kukipitisha chama tawala cha Bw Meles cha Ethiopian People's Revolutionary Democratic Front (EPRDF).
Bw Meles anatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuchaguliwa tena, huku upinzani ukionekana kugawanyika na kutokuwa na mpangilio mzuri.
BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment