MKAZI wa Kijiji cha Mkalamo wilayani hapa, Benny Barton (29)
anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba na kusababisha
kifo na majeruhi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Jaffar Mohamed alimtaja
aliyekufa kuwa ni mmiliki wa nyumba hiyo, Amiri Abdala (48).
Kwa mujibu wa Mohamed, tukio hilo lilitokea Mei 20 mwaka huu saa
5.00 usiku kijijini Mkalamo.
Mke wa marehemu, Lucia Albert (33) amejeruhiwa sehemu mbalimbali za
mwili. Kaimu Kamanda alisema mtuhumiwa anadaiwa kufanya kitendo hicho
kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni hasira ya kucheleweshwa kulipwa
fedha alizokuwa akiwadai wanafamilia hao baada ya kuwauzia baiskeli.
Alibainisha kuwa inadaiwa awali, waliuziana baiskeli kwa thamani ya
Sh 40,000. Inadaiwa kabla ya tukio hilo, wanafamilia hao walimlipa Sh
15,000, hatua iliyosababisha waendelee kudaiwa kiasi kilichobaki kwa
muda mrefu.
"Hawa jamaa baada ya kuuziana baiskeli kwa bei waliyokubaliana na
kutanguliza shilingi elfu kumi na tano, inadaiwa iliwachukua muda mrefu
kulipa deni linalowakabili mtuhumiwa baada ya kuona wanachelewa ndipo
aliamua kuwavizia wakiwa wamelala usiku na kuwasha moto nyumba hiyo kama
njia ya kufidia deni lake," alisema kaimu kamanda.
Abdala alikufa njiani wakati wanakijiji wakimkimbiza Hospitali ya
Wilaya ya Pangani. Mkewe amelazwa katika Hospitali ya mkoa wa Tanga ya
Bombo. Mtuhumiwa amezuiwa katika kituo kidogo cha polisi cha Pangani na
anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.
Habari Leo.
Monday, May 24, 2010
Atuhumiwa kumuua mdeni kwa kuchoma nyumba
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, May 24, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment