Naibu
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman
Jaffo akizungumza na uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe wakati
wa kupokea msaada wa Magodoro 60 kutoka NHIF.
“Katika hili NHIF mmefanya vizuri sana ….na sio hapa tu, nimekuwa nikipita katika
maeneo mbalimbali na taarifa zenu nakutana nazo kuwa mmekuwa wepesi sana katika
kushughulikia matatizo hasa ya uboreshaji wa huduma za afya pale mnapokutana
nayo,”
“Mmeboresha sana huduma zenu kwa wanachama wenu hasa kwa kupanua wigo wa
vituo vya kutolea huduma hatua inayowawezesha wanachama kupata huduma mahali
popote wanapotaka wao…sasa naomba viongozi wa halmashauri hakikisheni mnawapa
elimu watumishi na wananchi kwa ujumla juu ya huduma hizi za Mfuko,” alisisitiza
Naibu Waziri Jaffo.
Akitoa maelekezo ya mgao wa magodoro hayo, alimtaka Mganga Mkuu kutoa
kipaumbele katika Vituo vya Afya vya Mwanerumango, Masaki na Mzenga kwa kuwa
vina uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo.
======
Na Grace Michael
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman
Jaffo amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Waganga wa Wilaya kuhakikisha
wanatoa elimu ya umuhimu na matumizi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa
watumishi wengine ili waweze kunufaika na huduma hizo.
Mbali na hilo, ameupongeza Mfuko huo kwa jitihada ambazo umekuwa ukifanya katika
kushughulikia changamoto mbalimbali hususan za huduma za matibabu katika maeneo
yote wanapokutana nazo.
Hayo ameyasema wilayani Kisarawe wakati akipokea msaada wa magodoro 60 kutoka
NHIF ambao ambao umekabidhiwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo kwa lengo la
kusambazwa katika vituo vya afya ambavyo vina uhitaji mkubwa.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti, Rehani Athumani akitoa maelezo ya awali juu ya
misaada ambayo Mfuko umetoa katika maeneo mbalimbali.
Kwa upande wa NHIF, akikabidhi magodoro hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na
Utafiti Rehani Athumani alisema kuwa Mfuko ulibaini changamoto ya ukosefu wa
magodoro wilayani humo wakati ilipopita kwa ajili ya ugawaji mashuka hivyo Mfuko
ulidhamiria kuondoa tatizo hilo.
“Tulipita katika vituo mbalimbali wilayani hapa wakati tunagawa mashuka siku ya
sherehe za Uhuru ambapo Mfuko pia ulishiriki katika kufanya usafi katika vituo
hivyo…baada ya kuona tatizo hilo Uongozi wa Mfuko uliona kuna haja kubwa ya kubana
matumizi katika maeneo mengine kwa lengo la kuwasaidia wananchi,” alisema Bw.
Rehani.
Naibu Waziri akipata maelezo wodini.
Alisema kuwa jitihada za kubana matumizi zimeuwezesha Mfuko kutoa misaada ya
Magodoro 60 wilayani Kisarawe, mabati 400 katika zahanati ya Mpingi, Songea Vijijini,
Vitanda 20 na magodoro 20 katika kituo cha afya cha Mjimwema mkoani Ruvuma
pamoja na saruji tani tatu katika Shule ya Sekondari ya Kilangalanga.
“Mfuko huu ni wa Watanzania wote sisi tumepewa dhamana ya kuusimamia hivyo ni
lazima twende na kasi ambayo Rais wetu anaitaka kwa ajili ya kuwahudumia
Watanzania na niseme tu kwamba Huduma bora za Afya Tanzania inawezekana.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Elizabeth Omingo
akiongozana na Naibu Waziri (TAMISEMI) Seleman Jaffo wakati wa kupokea
msaada kutoka NHIF.
Naibu Waziri Jaffo akipokea msaada wa magodoro 60 kutoka NHIF.
Naibu Waziri Jaffo akisikiliza jambo kutoka kwa Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma Grace Michael.
Naibu Waziri akielezea mikakati ya Serikali ya awamu ya tano katika uboreshaji wa huduma.
Magodoro yakishushwa tayari kwa kupokelewa.
Waziri akiwa katika picha ya pamoja.
Kazi ikiendelea.
0 comments:
Post a Comment