SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 29, 2016

SEKTA BINAFSI ZAASWA KUTOA HUDUMA ZINAZOWANUFAISHA WAJASILIAMALI WADOGO.

KAMPUNI ya Aspro Capital Limited ni kampuni inayoingia ubia na wajasiliamali kwa kutoa huduma za kitalaam ili kuweza kutatua changamoto zinazomkabili mjasiliamali.

 Sekta binafsi  zaaswa kutoa huduma wanazotoa ziwanufaishe wajasiliamali wadogo kama serikali inavyotarajia na inavyofuatilia kwa karibu huduma zinazotolewa na sekta binafsi kwa wajasiliamali.

Hayo yamesemwa na 
Mkurugenzi wa Viwanda vidogo na biashara ndogo, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Consolatha Ishebabi wakati akizungumza na wajalisiamali waliokusanywa na kampuni ya 
Aspro Capital Limited jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa serikali imekuwa inafanya jitihada mbalimbali za kuendeleza wajasiliamali wadogo ikiwa ni pamoja kuanzisha mikakati na programu zinazolenga kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Aspro Capital Limited, Isaya Shoki amesema kuwa kampuni yao ni muunganiko wa wanahisa ili kusaidia wjsiliamali wadogo kwa upande wa vifungashio pamoja na masoko ya bidha za wajasiliamali wadogo.
Mkurugenzi wa Viwanda vidogo na biashara ndogo, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Consolatha Ishebabi akizungumza na wajasiliamali katika mkutano ulioandaliwa na Kampuni ya Aspro Capital Limited jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na uendelezaji wajasiliamali wadogo ambao wanataka kuendelez biashara zao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Aspro Capital Limited, Isaya Shoki akizungumza na wajasiliamali wadogo ambao wanafanya kazi za mikono katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Arch Financial & Investiment, Iyen Msemwa akifafanua jambo kuhusiana na Kampuni ya Aspro Capital Limited na jinsi inavyosaidia wajasiliamali hao 
Baadhi ya wajasiliamali wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Aspro Capital Limited jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Aspro Capital Limited, Isaya Shoki na Mkurugenzi wa Viwanda vidogo na biashara ndogo, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Consolatha Ishebabi wakiwa katika picha ya pamoja na wajasiliamali wadogo katika mkutano wa Kampuni ya Aspro Capital Limited jijini Dar es Salaam leo.

0 comments:

Post a Comment