Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ambaye ni Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akizungumza katika
ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji
katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya
Uwajibikaji Tanzania (WIPA) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar
es Salaam leo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ambaye ni Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh wakikata utepe
kuashiria ufunguzi
wa Kongamano la Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta
ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania
(WIPA) jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akikabidhiwa kibao maalumu mara baada ya kuzindua Kongamano
la Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi
na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ambaye ni Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh jijini Dar es
Salaam leo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja katika
Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji
Tanzania (WIPA) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango amesema kukosekana kwa
uwajibikaji na utawala bora kunafanya mfumo wa maisha ya wananchi
kuharibika.
Dk.Mpango
ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa
linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa
na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ,amesema katika kuweza
kufikia uchumi wakati lazima lipewe kipaumbele katika uwekezaji wa Gesi
na Mafuta.
Amesema jamii inayoamini uwajibikaji na utawala bora inafanya jamii hiyo kuwajibika kwa pamoja katika maendeleo ya kiuchumi.
Dk.Mpango
amesema akiwa Waziri mwenye dhamana ni kuangalia uwajibikaji kwa raia
katika nchi na bila kuangalia uwajibikaji na utawala bora mfumo wa
maisha ya wananchi unaharibika.
Amesema
taasisi ya wajibu ni moja ya taasisi ambayo itasaidia juu ya kutafsiri
wa uwajibikaji kwa wananchi kwa lugha inayofahamika na kueleweka.
Nae
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ambaye ni
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh amesema
nia ya kongamano hilo ni kutafuta mawazo ya watu wengine katika
uwajibikaji wa katika sekta ya Gesi na Mafuta.
Utouh
amesema kuwa kutokana na rasilimali hiyo kugundulika wameona kuna
umuhimu wa kushirikisha watu wengine ambao walipata rasilimali hiyo
lakini hakuweza kuwasaidia ambapo hata Tanzania tunaweza kuangukia huko.
Mkutano
huo umeshirikisha watu waliobobea katika sekta ya Gesi na Mafuta katika
kutoa mawazo yao juu ya Tanzania inavyoweza kufanya katika sekta hiyo.
0 comments:
Post a Comment